Kikundi cha ngoma kutoka nchini Rwanda kikitumbwiza kwenye jukwaa katika tamasha la JAMAFEST 2019 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Kikundi cha ngoma kutoka nchini Kenya kikitumbwiza kwenye jukwaa katika tamasha la JAMAFEST 2019 uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaa
Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Burundi Katika tamasha la JAMAFEST 2019
Baadhi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye maonyesho ya JAMAFEST 2019 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Mabanda ya Wajasiriamali ya nguo na viatu katika maonyesho ya JAMAFEST 2019
Moja ya mabanda ya vinyago katika tamasha la JAMAFEST 2019
Moja ya mabanda ya nguo na picha za kuchora katika tamsha la JAMAFEST 2019
Moja ya kikundi kiwakilishi kutoka nchini Tanzania kikitumbwiza katika maonyesho ya JAMAFEST 2019 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Moja ya kikundi kutoka nchini Zanzibar kikitumbwiza katika jukwaa kwenye maonyesho ya JAMAFEST katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Slivia Sebastian, Baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania 2019 jijini Dar es salaam
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia Bodi ya Sanaa wamekutana na wasanii kutoka kada mbalimbali na kujadili changamoto na namna ya kuzitatua ili kuweza kuipeleka mbele tasnia hiyo ambayo inachangia pato la taifa kwa asilimia 13.5.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Mh. Dkt. Harisson Mwakyembe akizungumza na wasanii na wadau wa sanaa.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya
Mwaka 1984.Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa
Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka
1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini
Dira
Kuwa chombo chenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa huduma bora kitaifa katika maendeleo ya sanaa
Lengo kuu
Kufufua, kukuza na kuongeza maendeleo ya utengenezaji wa kazi bora za sanaa.
Maadili
Maadili ya msingi ya Baraza la Sanaa la Taifa ni kuhimiza na kukukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania,
kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu na kuchochea ubunifu na uvumbuzi katika sanaa
Limepania kuhimiza na kukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania
Limepania kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu
Limepania kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika sanaa