Habari na Matukio

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe: 03/04/2015

BASATA YAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO NA UKIUKAJI WA SHERIA ZA UENDESHAJI KUMBI ZA BURUDANI KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU YA PASAKA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

Read more...TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe: 31/03/2015

WASANII WATAKIWA KUHIFADHI KAZI ZAO, KUMBUKUMBU
Na Mwandishi Wetu

Wasanii nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuhifadhi kazi zao na kumbukumbu mbalimbali zinazowahusu ili kuepuka kupotea, kusahaulika na kuwezesha kuzirithisha kwa vizazi vijavyo.

Read more...Tarehe: 03/03/2015

BASATA KUENDESHA PROGRAM YA MAFUNZO YA SANAA KWA WATOTO WAPATAO 215 KUTOKA WILAYA YA TEMEKE MKOA WA DAR ES SALAAM.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa kwa kushirikiana na taasisi ya Ako'mungoma Poverty Alleviation Organization (APAO) linaendesha programu ya wiki tatu ya Sanaa kwa watoto katika Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Read more...BASATA YATOA ELIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA WASANII

Na Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia programu yake ya Jukwaa la Sanaa wiki hii limetoa elimu kwa wasanii kuhusu maudhui ya katiba inayopendekezwa hasa ibara ya 59 ya katiba hiyo inayohusu sekta ya Sanaa.

Read more...TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHESHIMIWA CAPTAIN JOHN DAMIAN KOMBA (MB)

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Captain John Damian Komba kilichotokea jioni ya Jumamosi ya tarehe 28/02/2015.
Captain John Damian Komba ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.

Read more...TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mke wa Msanii mkongwe wa muziki wa dansi na Mjumbe wa Bodi ya BASATA Bw. John Kitime kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa kuamkia Ijumaa ya Tarehe 13/02/2015.


Aidha, BASATA linatoa salamu rambirambi kwa kifo cha Baba Mzazi wa Msanii Dully Sykes, Mzee Abby Sykes kilichotokea jana Jumapili ya Tarehe 15/02/2015.

Read more...TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

GODFREY L. MNGEREZA ATEULIWA KUWA KATIBU MTENDAJI WA BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kuwatangazia Wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amemteua ndugu Godfrey Lebejo Mngereza kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Read more...BASATA YAHIMIZA MSHIKAMANO WA WASANII

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujenga ushirikiano kupitia vyama na mashirikisho yao ili kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na unaoeleweka wa uendeshaji wa tasnia ya sanaa nchini.
Read more...

Copyright © 2014. All Rights Reserved.