Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

Hawa hapa wanaowania tuzo za TMA2023

10 Sep, 2024
Hawa hapa wanaowania tuzo za TMA2023

Hawa hapa wanaowania tuzo za TMA2023

Isack N. Bilali.

Dirisha la kuwapigia kura wanamuziki watakaowania Tuzo za muziki Tanzania (TMA) limefunguliwa rasmi tarehe 03 Septemba, 2024 saa 5 usiku mara baada ya kamati inayoratibu TMA chini ya uenyekiti wa David Minja na Makamu mwenyekiti Seven Mosha kuweka wazi vipengele vyote vinavyoshindaniwa na wasanii mbalimbali.

Kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka wanaowania ni Marioo wimbo wa “Shisha”, Diamond “Shuu”, Harmonize “Single again”, Ali Kiba “Sumu” na mwisho ni Jay Melody na wimbo wake wa “Nitasema”.

Aidha, Kipengele cha mwanamuxziki bora wa kike wa mwaka wanaowania ni Zuchu “Honey”, Anjela “Blessing”, Malkia Leyla Rashid “wat una viatu” na Nandy “Falling”.

Kwa upande wa Bongo fleva mwimbaji bora wa kiume wa mwaka kinashindaniwa na Diamond “Yatapita”, Jay Melody “Sawa”, Alikiba “Mahaba”, Marioo “Love Song” na Harmonize “Single again”.

Mwimbaji bora wa kike wa bongo fleva wa mwaka ni Zuchu “Naringa”, Appy “Watu feki”, Nandy “Falling”, Phina “Sisi ni wale” na Anjela “Blessing”.

Kwa upande wa wimbo bora wa ushirikiano wa mwaka wanaochuana katika kipengele hiki bni Alikiba ft. Marioo “Sumu”, Mboso ft. Chley “Sele”, Abigail Chams ft. Marioo “Nani”, Jux ft. Diamond “Enjoy” na Diamond ft. Koffi Olomide “Achii”.

Katika kipengele cha Albamu bora yam waka walioingia katika mchuano ni Abigail Chams “5”, D Voice “Swahili Kid”, Navy Kenzo “Most People Want this”, Harmonize “Visit Bongo” na Ray Vanny “Flowers III”.

Mwanamuziki bora chipukizi wa mwaka wanaoshindania nafasi hiyo ni Pamoja na Xouh “Lalala”, Chino Kid “Gibela”, Appy “Watu feki”, Mocco Genius “Mi Nawe” na Yammi “Namchukia”.

Mtifuano wa ngumu kumeza katika wimbo bora wa HipHop wa mwaka unapigwa vikali na wasanii kama Rapcha “Uongo”, Country Wizzy “Current situation”, Young Lunya “Stupid”, Stamina ft Bushoke “Machozi” na Joh Makini “Bobea”.

Mwimbaji bora wa Hip Hop ni Young Lunya “Stupid”, Kontawa “Dunga mawe”, Stamina “Machozi”, Joh Makini “Bobea” na Rosa Ree “Mama Omollo”.

Huku Mtozi bora wa muziki wa Hip hop wa mwaka wanaowania kipengele hicho ni Black Beatsa “Warrior”, S2Kizzy “Maokoto”, Ommydaddy “Wanangu kibao”, Ringle beatz “Tribulation” na Dupy Beatz “Mr. Christmas part 5”.

Kipengele cha Dj bora wa mwaka katika tuzo za TMA kinashindaniwa na Dj D Ommy, Dj Seven Worldwide, Dj Shana Mnyamwezi, Dj Hijab na Dj Mamie. Upande wa utumbuizaji bora wa kike wa mwaka waliotajwa ni Zuchu “Nani remix”, Phina “Do Salale”, Abigail Chams “Milele” na Da Princess “Lolo”.

Mtumbuizaji bora wa kiume wa mwaka kipengele hiki kinawaniwa na Mboso “Sele”, Christian Bela “Tamu”, Harmonize “Single again”, Alikiba “Sumu” na Diamond “Shu”.

Mtunzi bora wa muziki wa dansi wa mwaka inawaniwa na wanamuziki wafuatao Master Keys, Dad One Touch, Erast o Mashine, na Christian Bela. Juu ya hapo mwandishi bora wa mwaka waliowekwa katika ushindani ni Pamoja na Mbosso, Dulla Makabila, Thabit Abdul, Jay Melody na Marioo.

Mtozi bora wa muziki wa bongo fleva wa mwaka wanaoshindanishwa ni Ibrah Jacko, Aloneym, Trone, S2Kizzy, na Mr. L huku wanaowania tuzo ya Mtozi bora wa muziki wa mwaka wakiwemo S2Kizzy, Mr. LG, Laizer, Thabit Abdul na Trone.

Mwongozaji bora w avideo wa mwaka ni Hanscana “Maokoto”, Nicklass “Dungamawe”, Ivan “Sele”, Folex “Achii” na Director Wayan “Huku”.

Mwanmuziki bora wa mwaka wa nyimbo za asili wanaowania ni Elizabeth Malinganya “Boda boda”, Erica Lulakwa “Aragoba”, Sinaubi Zawose ”Peasa”, Ngapi group “berita” na Wamwiduka band “Usizime Muziki”.

Wanaowania wimbo bora wa mwaka wa asili ni Sinaubi Zawose ”Peasa”, Man Fongo na Nyati group “Sauti ya Kumoyo”, Erica Lulakwa “Aragoba”, Wazawa music band “Muziki hauna mwenyewe” na Wamwiduka band “Usizime Muziki”.

Mwimbaji bora wa muziki wa dansi wa mwaka ni Christian Bella “Kanivuruga”, Melody Mbassa “Hellena”, Papi Kocha “Jela ya Mapenzi”, Charlz Baba “Mmbeya” na Sarah Masauti “Popo”.

Wimbo bora wa dansi wa mwaka wanaowania ni Diamond ft Koffie olomide “Achii”, Melody Mbassa “Nyoka”, Malaika Band “Kanivuruga” na Twanga pepeta “Mmbea”.

Kwenye upande wa mwanamuziki bora wa dancehall wa mwaka wanaowania nafasi hiyo ni Pamoja na Dj Davizo “Dance hall”, Badest 47 “Zagamua”, Appy “Mr Hatter”na Bayo the great “Nakupenda”. Upande wa wimbo bora wa Dance hall wa mwaka unashindaniwa na Planner “You”, Dj Davizo “Dance hall”, Badest 47 “Zagamua”, Appy “Mr Hatter”na Bayo the great “Nakupenda”.

Sanjari na vipengele vilivyotajwa hapo mwanzo pia kuna kipengele cha mwanamuziki bora wa Reggae wa mwaka ambacho kinawaniwa na Akilimali “Africa Mama”, Dipper rato “Grateful”, Dimateo zion “Rhymes tonight”, Ras Nono “Andika” na Warrior from the East “Wewe”.

Wimbo bora wa reggae wa mwaka wanaowania ni Warriors from the East “Wewe”, Akilimali “Africa Mama”, Dimateo zion “Rhymes tonight”, Mr Kamanzi “Give and Thanks” na Paul Mihambo “Salamu zako”.

Kwa upande wa taarab vipo vipengele vitatu ambavyo ni Mtunzi bora wanaowania ni Father Mauji “umenibamba”, Bob Rama “Nkurumbi”, Babu Juha “Kisaka”, Thabit Abdul “DSM Sweetheart” na Mfalme Mzee Yusufu “Sina Wema“  Huku, Mwimbaji bora wa mwaka inawaniwa na Salha “DSM Sweetheart”, Mwinyimkuu “Bila yeye sijiwezi”, Malkia Leyla Rashid “Watu na Viatu”, Amina Kidevu “Hatuachani” na Mwansiti Mbwana “Sina wema”.

Wimbo bora wa taarab wa mwaka unawaniwa ni Malkia Leyla Rashid “Watu na Viatu”, Salha “DSM Sweetheart”, Mwansiti Mbwana “Sina wema”, Mwinyimkuu “Bila yeye sijiwezi” na Amina Kidevu “Hatuachani”.

Tuzo nyingine inaenda katika kipengele cha Mtanzania anayeipeperusha vema bendera ya Tanzania Kimataifa (Tanzania Global Icon Award) wanaowania Tuzo hii ni Pamoja na Mchezaji mpira wa miguu Mbwana Samatta, Mwanamitindo Flaviana Matata, Wanasarakasi Ramadhan Brothers Pamoja na Anisa Mpungwe na Clara Luvanda.

Kipengele cha video bora ya muziki yam waka inashindaniwa na Billnass “Maokoto”, Mbosso “Sele”, Zuchu ft Innos B “Nani remix”, Diamond ft Koffie Olomide “Achii” na Harmonize “Single Again”.

Turufu ya wimbo bora wa mwaka inachezwa na wasanii wafuatao Zuchu “Honey”, Harmonize “Single Again”, Jux ft Diamond “Enjoy”, Lavalava “Tajiri” na Diamond “Shu”. Kamati hiyo imetaja kipengele cha mwisho kuwa ni “Best song East west and southern Africa” wanaowania ni Libiana “People”, Qing Madi “American Love”, Asake “Lonely at the top”, David ft Musa Keys “Unavailable” na Tyler ICU and Tumelo ft Dj Maphorisa “Mnike”.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo imeweka wazi kuwa upigaji kura utafikia tamati tarehe 28 Septemba, 2024 hivyo wadau wa sanaa waendelee kuwapigia kura wanamuziki katika vipengele walivyotokea kushindania huku usiku wa tuzo za muziki Tanzania ukitarajiwa kufanyika tarehe 29 Septemba, 2024.

Settings