Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa
Kuwajibika kwa shughuli za kila siku na usimamizi wa Kurugenzi ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa. Idara inaongozwa na mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Ukuzaji na maendeleo ya Sanaa na kusimamia sehemu nne, ambazo ni;
Sehemu nne;
- Sehemu ya sanaa za Maonesho
- Sehemu ya sanaa za Ufundi
- Sehemu ya Utafiti na Masoko
- Sehemu ya Muziki.
Majukumu
- Kumshauri Katibu Mtendaji kuhusu masuala yanayohusu ukuzaji na maendeleo ya sanaa
- Kuandaa mikakati ya kukuza na kuendeleza sanaa
- Kuratibu shughuli za muziki, Sanaa za ufundi na Sanaa za maonesho;
- Kudhibiti ubora na viwango vya kazi ya sanaa
- Kutoa ushauri wa kiufundi kwa wasanii na wadau wa sanaa kuhusu Muziki, Sanaa za Maonyesho, Ufundi na Utafiti na Masoko
- Kutambua na kusajili wasanii na wadau wa sanaa
- Kutangaza kazi za sanaa kwa wasanii waliosajiliwa, vikundi vya sanaa, vyama vya sanaa, mashirikisho ya sanaa na wadau wa sanaa
- Kufanya utafiti, uhifadhi wa kumbukumbu za matukio ya wasanii kwa wasanii binafsi waliosajiliwa, vikundi vya sanaa, vyama vya sanaa, mashirikisho ya sanaa na wadau wa sanaa;