Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma
Kuwajibika kwa shughuli za kila siku za Mawasiliano na Uhusiano wa Umma
Majukumu
- Kuandaa, kushiriki na kufuatilia Mkakati wa Mawasiliano na Utetezi wa Baraza
- Kuimarisha na kudumisha uhusiano mzuri wa umma kwa wateja na wadau wa sanaa;
- Kuandaa na kuratibu mikutano ya Baraza na waandishi wa habari;
- Kutayarisha taarifa ya Baraza kwa vyombo vya habari kuhusu masuala ya kisanii; na
- Kudumisha na kusasisha habari kwenye tovuti ya Baraza na majukwaa yake ya mitandao ya kijamii; na
- Kufanya kazi nyingine yoyote inayohusiana kama itakavyoagizwa na msimamizi.