Historia
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019. Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini
Kazi za Baraza
Kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019, ambayo kwayo Baraza liliundwa, Majukumu ya Baraza ni pamoja na :
Muundo wa Baraza
Baraza la Sanaa la Taifa lina wajumbe wa Baraza ambao uteuliwa na Waziri anayehusika na masuala ya Sanaa. Mwenyekiti wa Baraza uteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Baraza uteuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu. Wakati ambapo vipindi vya kuteuliwa kwa wajumbe havina ukomo, uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza ni kwa vipindi viwili tu vinavyofuatana. Kwa kawaida wajumbe wa Baraza uteuliwa kwa msingi wa uwakilishi wa mikoa, asasi, asasi zinazofundisha Sanaa, idara za Serikali na asasi zisizo za Serikali.
Baraza linaongozwa na Katibu Mtendaji, ambaye ndiye Afisa mtendaji mkuu. Baraza lina idara Mbili zifuatazo:
Licha ya idara hizo Mbili, kuna vitengo vitano ambavyo hufanya kazi moja kwa moja chini ya Katibu Mtendaji. Vitengo hivyo ni ;
Sanaa hujumuisha
Ambao unaweza kuwa wa kuimba na wa vyombo uliorekodiwa kwa sauti au utunzi wa muziki ulioandikwa, bendi, muziki wa jazi, ala, uliorekodiwa, video, taarabu, kwaya, gwaride,muziki wa asili wa ngoma na unaoambatana na maigizo na thamthiliya.
Hujumuisha picha za kuchorwa kwa rangi, uchoraji wa kawaida, michoro ya majalada, vitabu au magazeti, uchoraji wa kwenye vitu vigumu kama metali au mbao, uandishi wa herufi ulionakishiwa, sanaa za vikaragosi kwa kutumia kompyuta na michoro iliyochapishwa. Ramani, michoro ya majengo na vielelezo, sanaa za kuumba na kuchonga, picha mgando za kamera, Kazi za usanifu majengo katika maumbo Sanaa za viwandani ikiwa pamoja na zilizo katika picha au zilizofumwa na urembo, na ubunifu wa mavazi, ususi na useketaji wa nguo.
Michezo ya kuigiza ya jukwaani, maigizo bubu, usanifu wa majukwaa, maleba, mapambo, uandishi wa tamthiliya, ngoma na ubunifu wake, sauti na vifaa vya jukwaani, sarakasi za binadamu au za wanyama, michezo ya redio.