Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kusimamia Ukaguzi wa Ndani wa Fedha na Utendaji na kutoa hakikisho kwa Bodi ya Wadhamini na Menejimenti juu ya uthabiti na utoshelevu wa udhibiti wa ndani na muundo wa utawala.
Majukumu
Kusaidia wakaguzi wa nje wakati wa shughuli za ukaguzi wa Halmashauri;
Kutayarisha ripoti za ukaguzi wa mara kwa mara kwa matumizi rasmi ya ndani na nje;
Kusaidia menejimenti kujibu hoja za ukaguzi zilizoibuliwa;
Kumshauri Katibu Mtendaji kuhusu masuala ya Ukaguzi wa Ndani;
Kufanya shughuli za ukaguzi wa ndani;
Kusimamia na kutathmini uzingatiaji wa Baraza katika kanuni za fedha na manunuzi;
Kufanya kazi nyingine yoyote inayohusiana kama itakavyoagizwa na msimamizi.